Saturday, August 27, 2016

PICHA ZA MATUKIO MBALI MBALI - MISS ILALA TALENT SHOW-26 AUG 2016

Chief Judge akisoma matokeo ya walioingia Tano bora

Mwalimu na vilevile ndie aliekuwa Mc wa shindano hili la kumtafuta mrembo mwenye kipaji.

Hapa ni Ukumbi wa High Spirit kwa ndani ambao siku hii ya leo ulikuwa unatumika kama sehemu ya kwanza ya kupumzika na kupata moja mbili wakati unasubiria program zingine ziendelee za kumtafuta malkia mwenye kipaji. 

Atsoko ni moja kati ya wawezeshaji wa mchuano huu wa kumtafuta malkia wa Ilala kwa mwaka 2016 na leo walikuwepo hapa High Spirit jengo la IT Plaza kuhakikisha warembo wanakuwa na muonekano mzuri kabisa.

Wadau wakifuatilia mchuano kwa makini zaidi

Baadhi ya wadau ya masuala ya urembo na mitindo wakishuhudia mpambano mkali wa warembo, wakichuana kutwaa taji la mwenye kipaji.

Mratibu wa Miss Dar City Centre 2016 Nancy au Super Model akiwa na mwenzake wakifuatilia kwa karibu mchuano wa kumtafuta malkia mwenye kipaji...Miss Ilala 2016 Talent Show 
Warembo wa Ilala mwaka 2016 wakiwa mbele ya majaji wakisiliza matokeo yao nani kawa nani nani kapita nani kabaki..Talent Show

Warembo wa Miss Ilala 2016 wakiwa katika picha ya pamoja ya utambulisho kabla ya kuanza kwa mchuano wa kumtafuta malkia mwenye kipaji kupita wenzake.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.