Saturday, August 27, 2016

WAREMBO WATANO WA ILALA WENYE VIPAJI

Hawa ndio warembo watano wenye vipaji ambavyo mshindi kati ya hawa atatangazwa siku ya fainali ya kumpata mrembo wa Ilala kwa mwaka 2016 katika ukumbi wa Hotel ya Nyota tano Hyatt Regency-Kilimanjaro Hotel kwa kiingilio cha Tshs.100,000 kwa viti maalum na Tshs 50,000 kwa viti vya kawaida, pia kutakua na burudani mbalimbali.

PICHA ZA MATUKIO MBALI MBALI - MISS ILALA TALENT SHOW-26 AUG 2016

Chief Judge akisoma matokeo ya walioingia Tano bora

Mwalimu na vilevile ndie aliekuwa Mc wa shindano hili la kumtafuta mrembo mwenye kipaji.

Hapa ni Ukumbi wa High Spirit kwa ndani ambao siku hii ya leo ulikuwa unatumika kama sehemu ya kwanza ya kupumzika na kupata moja mbili wakati unasubiria program zingine ziendelee za kumtafuta malkia mwenye kipaji. 

Atsoko ni moja kati ya wawezeshaji wa mchuano huu wa kumtafuta malkia wa Ilala kwa mwaka 2016 na leo walikuwepo hapa High Spirit jengo la IT Plaza kuhakikisha warembo wanakuwa na muonekano mzuri kabisa.

Wadau wakifuatilia mchuano kwa makini zaidi

Baadhi ya wadau ya masuala ya urembo na mitindo wakishuhudia mpambano mkali wa warembo, wakichuana kutwaa taji la mwenye kipaji.

Mratibu wa Miss Dar City Centre 2016 Nancy au Super Model akiwa na mwenzake wakifuatilia kwa karibu mchuano wa kumtafuta malkia mwenye kipaji...Miss Ilala 2016 Talent Show 
Warembo wa Ilala mwaka 2016 wakiwa mbele ya majaji wakisiliza matokeo yao nani kawa nani nani kapita nani kabaki..Talent Show

Warembo wa Miss Ilala 2016 wakiwa katika picha ya pamoja ya utambulisho kabla ya kuanza kwa mchuano wa kumtafuta malkia mwenye kipaji kupita wenzake.

MISS ILALA 2016 @HYATT REGENCY-KILIMANAJRO

JIHAN DIMACHK MISS ILALA 2014-2015, JE NANI ATAMPOKEA TAJI HILO 2016..KWA KIINGILIO CHA TSH 100,000 KWA VITI MAALUM NA TSH 50,000 VITI VYA KAWAIDA UTAAMSHUHUDIA MALKIA MPYA WA ILALA..WAKISINDIKIZWA NA BURUDANI MBALIMBALI

Wednesday, October 1, 2014

REDD'S MISS TANZANIA 2014 SPORTS DAY BONANZA AND CHARITY

Karibuni sana wadau wote wa michezo tucheze na warembo wetu wa Tanzania, pamoja na watoto wetu, kutakuwa na michezo mbali mbali kwa ajili ya wakubwa na watoto karibuni sana, escape one tarehe 5 Jumapili, Oktoba, 2014 kuanzia asubuhi mpaka mida ilee...

Tuesday, May 20, 2014

MISS DAR CITY CENTRE 2014 @ DAR ES SALAAM FREE MARKET

Tunawaomba msamaha kwa mabadiriko yaliyotokea ya eneo la kufanyia shughuli ya Miss Dar City Centre 2014, Mwanzo ilikuwa Escape One na Sasa tunafanyia Dar es Salaam Free Market (Century Cinema) karibu na ubalozi wa Kenya.
Asante kwa ushirikiano wako, tunaomba mje kwa wingi tushuhudie nani ni nani kwenye mchuano huu kabambe.

Thursday, May 15, 2014

WAREMBO WAKIHOJIWA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA SIKU YAO YA VIPAJI


    Baadhi ya warembo wakiwa katika pozi la pamoja.   Warmbo wakifanya mahojiano na mwaandishi wa Clouds Tv

    
     
Mratibu wa mashindano ya Miss Dar City Centre 2014 Judith Charles akihojiwa na waandishi wa   habari, kushoto ni mmoja wa wazamini wa Miss Dar City Centre 2014 Marketing Manager wa Maisha Club Gilla Geofrey, Upande wa kulia ni Mwalimu Msaidizi wa warembo Thureya


Baadhi ya warembo wakiwa katika pozi.